Ticker

6/recent/ticker-posts

AINA 10 ZA VYAKULA VINAVYO MFAA MAMA MJAMZITO NA MTOTO ALIEPO TUMBONI


AINA 10 ZA VYAKULA VINAVYO MFAA MAMA MJAMZITO NA MTOTO ALIEPO TUMBONI.

Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini.

Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku. Mama mwenye ujauzito anapaswa kula vizuri kwa ajili ya afya yake na mtoto aliye tumboni.  Mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora. 

Sanihealth iliweza kukundalia vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula ambavyo ni pamoja na:-

1. Jamii ya kunde mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. 

Sanihealth: https://sanihealthtz.blogspot.com/2023/03/kwanini-sibebi-mimba-wakati-sina-tatizo.html

Tufuatilie kwenye Instagram facebook na Twitter. Pata habari muhimu zaidi kwenye blog yetu uipendayo! 

Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii ya kunde zinatosheleza mahitaji ya protini. Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya,Peas,Karanga, Alfa alfa,kunde, maharage. 

2. Mayai Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi ya magonjwa mbali mbali. 

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi. 

Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli, Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo. 

4. Viazi vitamu Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto,ngozi na mifupa.

5. Nyama ya nguruwe,kuku au ngombe huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne na kuendelea.

6. Nafaka na vyakula vya Wanga Vyakula hivi huupa mwili nguvu ya kufanya kazi na ukuaji wa mtoto tumboni. Vyakula hivi ni kama mahindi,mtama ,mihogo, vyakula vya ngano kama mkate  n.k.

7. Avocado parachichi ni tunda ambalo lina mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Parachichi linasaidia katika ukuaji wa ubongo,ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni. 

8. Mboga za majani Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha. 

Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia. 

9. Mafuta ya samaki Mafuta ya maini ya samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto. 

10. Maji Maji ni muhimu kwa mwili kwasababu yanasaidia kwenye mmeng'enyo na unyonywaji wa viinilishe pia husaidia kuzuia choo kigumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)

Sanihealth (Afya BoraTanzania) ndio chaguo sahihi kwaajili ya kuboresha afya ya mama na mtoto tumboni kwa mawasliano zaidi na ushauri bonyeza hapa chini.

wa.me/255658091941 

Kwa mafunzo zaidi na maswali  kuhusu Afya weka coment yako hapa chini ili kukata kiu ya mafunzo ya Afya ya Mama na Mtoto.

Chapisha Maoni

0 Maoni