Ticker

6/recent/ticker-posts

UMUHIMU WA HOMONI 4 NA KAZI ZAKE

 


Wengi wetu hatufikirii juu ya homoni katika maisha yetu ya kila siku. Tunajua kwamba kuna homoni katika miili yetu, mabadiliko ya homoni kwa wavulana na wasichana wanapobaleghe.

Wanawake wanasadikiwa kuwa na ‘hormonal’ angalau mara moja wakiwa na hedhi

Wengi wetu tunajua angalau jukumu la testosterone na estrojeni katika ukuaji wa binadamu.

Homoni huendesha kila kitu maishani mwetu – ndio maana wakati mwingine unajisikia vizuri, wakati mwingine unajisikia vibaya, wakati mwingine unakasirika, yote haya hutokana na mabadiliko ya homoni.

HOMONI NI NINI, NA ZINATOKA WAPI?


Homono ni (“kichochezi”,ama “msukumo”)

Ni kemikali zinazotolewa na tezi za mwili na kusafiri kupitia mfumo wa mzunguko wa damu hadi ogani za mwili. Humo zinasababisha mabadiliko katika kazi ya ogani.

Mwili wetu huwasiliana na yenyewe kupitia homoni. Tezi ya pituitari, tezi, ya adrenalini, ovari na korodani zote ni sehemu ya shirika hili. Kwa ujumla kuna viungo vingi visivyojulikana. Ushawahi kujiuliza jinsi akili na miili yetu hufanya kazi pamoja. Hiyo ndiyo sababu mojawapo iliyonifanya kuwa tabibu.

Kazi za homoni inachangia karibu kila tabia katika maisha yetu, lakini huenda tusiwe na ufahamu wa kile kinachotokea.

Kwa mfano, unapofanya mazungumzo na watu wako wa karibu, je, unahisi upendo na kuongezeka kwa hisia ya furaha?

Hali hiyo inachangiwa na homoni inayojulikana kama oxytocin. Inahimiza tabia zinazoimarisha uhusiano wa kifamilia.

Je, unajisikia kuwa na nguvu na kuridhika unapokimbia?

Hali hiyo inachangiwa na homoni ya endomorphin. Wakati huo ufahamu wako wa maumivu hupungua na hisia za furaha huongezeka.

Maisha yetu yangelikuwa vipi ikiwa tungefanya mambo yanayochangamsha homoni kimakusudi, badala ya kungoja homoni kutolewa kwa njia za kiasilia za maumbile tunapofanya mambo yanayotufanya tujisikie vizuri?

Na je hali ingelikuwa vipi iwapo ungechochea homoni hizo katika kazi yako, wakati wa tafrija na katika mahusiano ili kuwa na afya njema? Bila shaka tungelikuwa na uwezo wa mkubwa wa kuishi kwa furaha nyakati zote.

Zifuatazo ni homoni 4 unazotakiwa kuimarisha ili kuwa na furaha:

Oxytocin
Oxytocin ni homoni muhimu ya ‘upendo’ ambayo itaboresha uhusiano wako kimwili.

Homoni hii hutolewa unapojisikia salama, unapo jumuika na watu wengine au kuwa karibu na watu katika imani yako. Madhumuni ya homoni hii ni kuimarisha uhusiano kati ya wanadamu, ili wazazi waweze kuwa karibu na watoto wao, kudumisha muundo wa familia na kusaidia wanandoa kupata ukaribu zaidi.

Ili kuchochea homoni hizi kiasili: Cheza na wanyama wanaofugwa wanaofugwa nyumbani kama vile sungura au paka na mbwa.

Watendee hisani marafiki au familia kwa upendo
Unapaswa kuthaminiwa
Mazungumzo ya ana kwa ana na umpendaye Jikande au upate mtu akukande
Andaa chakula na ule na uwapendao.

Serotonin
Ni homoni inayofanya kazi nyingi sana mwili , homoni hii hujulikana kama homoni ya utulivu kwa sababu homoni hii huweza kuchochea mtu kuwa na utulivu.

Wataalamu wanashauri kuwa mazoezi ya misuli ni muhimu katika kuimarisha mifupa ya mwili hasa unapoongeza shinikizo kwa mifupa yako kwa njia ya mazoezi. Hufanya kazi kama homoni na kama mjumbe(nyurotransimita) wa taarifa. Husafirisha ujumbe kati ya seli moja ya neva na nyingine. Serotonin huzalishwa katika utumbo, ubongo, mfumo wa neva na chembechembe hai za damu. Homoni hii imehusishwa na udhibiti wa hisia, usingizi wa usawa, furaha na wasiwasi.

ILI KUCHOCHEA HOMONI HIZI KWA KIASILI:


Simama kwenye jua kwa muda kidogo Kimbia, ogelea au endesha baisikeli Chukua muda wako kutafakari mambo
Tembea katika mandhari ya kupendeza.

Dopamine. Hii ni homoni kuwajibika kwa hali ya kisaikolojia ya hisia ya mtu. Inasaidia utendaji kazi wa moyo na ubongo, husaidia kudhibiti uzito na kuwajibika na utendaji. Inahamasisha mwili wetu kupata zaidi (motisha ya kupata zaidi katika suala la chakula na mafanikio ni muhimu.

Ukosefu wa homoni hii katika mwili wa binadamu husababisha hali huzuni ya mara kwa mara na mkusanyiko wa uzito kupita kiasi.

ILI KUCHOCHEA HOMONI HIZI KWA KIASILI:-


Kula chakula unachopenda
Sherehekea ushindi mdogo katika maisha ya kila siku
Jitunze Sikiliza muziki mzuri
Unapaswa kukamilisha kazi au mradi ambao umeanzisha.

Endorphins
Homoni ya endorphin ni dawa ya asili ya kutuliza maumivu. Inasaidia kutibu maumivu, kupunguza msongo wa mawazo, na kuongeza furaha.

Unapokula chakula homoni ya endorphins’ hutolewa, hivyo huufanya ubongo wako ujisikie furaha. Endorphins ni homoni maalum ambayo ikiwepo ya kutosha humfanya mtu kujisikia raha.

OXYTOCIN, SEROTONIN, DOPAMINE, ILI KUCHOCHEA HOMONI HIZI KIASILI:


Fanya mazoezi
Cheza na marafiki au tazama/ sikiliza vipindi vya vichekesho
Kula chokoleti Maono ya kisanii yanapaswa kudumishwa

Jaribu kutumia mafuta kama vile lavender, machungwa, au ubani,. Na bila shaka ngono. Kwa hivyo, kufanya ubongo na mwili wako kujisikia katika hali nzuri, ni vyema kuzingatia baadhi ya mienendo kila siku ili kuchochea homoni zinazohitajika.

Chapisha Maoni

0 Maoni