Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO WA KIKE AU WA KIUME.


JINSI YA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO WA KIKE AU WA KIUME.

Je, nikweli unaweza kuchagua Jinsia ya mtoto wako?

Ndi uwezekano wa kuchagua jinsia ya mtoto unaemtaka upo kwa kuchagua njia hii na baadhi ya wanandoa wamethibitisha hilo kwa kufuata utaratibu huu.

Kuanzia uchaguzi wa vyakula, hadi wakati wa kushiliki tendo la ndoa, hata nafasi za kushiliki tendo la ndoa. Kuna madarasa maarumu kadhaa na mawazo yanayoweza kuwa na mchango wa kukusaidia kuchagua jinsia ya mtoto wako. 

Katika chapisho hili tutagusa sayansi nyuma ya mada hii kwa kuhakiki kama unaweza kuchagua kupata mvulana au msichana.

Kabla ya kuzama katika mada hii yenye utata, tunataka kuwa wazi kuwa jinsia na jinsia ni tofauti. Katika makala hii, tunazungumzia kuhusu kupata mimba ya mwanamume au mwanamke.

Siku za kupata mtoto wa kiume Watu wengi hutamani kupata mtoto wa jinsia wanayoipenda. 

Nini nifanye ili nipate mtoto wa kike au kiume? 

Je kuna dawa au vyakula vya kusaidia kupata mtoto ninayemtaka?

Siku gani nikikutana na mwenzangu naweza pata mtoto wa kiume au kike? 

Na maswali mengine mengi huonesha shauku kubwa ya kupata mtoto wa jinsia uipendayo.

Jinsia ya Mtoto

Mtoto hutengenezwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la kike. Mbegu za kiume hubeba vinasaba vya X na Y, wakati yai la mwanamke likiwa na vinasaba vya X peke.

Ikikutana mbegu ya kiume yenye kinasaba cha X na yai la kike (yenyewe yana vinasaba vya X peke yake) mtoto wa kike hutungwa. Mbegu ya kiume yenye kinasaba cha Y Ikikutana na yai la kike, mtoto wa kiume hutungwa.

Mbegu ya kiume Y + Yai la kike X = Mtoto wa Kiume

Mbegu ya kiume X + Yai la kike X = Mtoto wa Kike

Njia za Kupata Mtoto Wa Jinsia Uipendayo

Mtoto wa kiume

Mbegu za kiume zenye vinasaba vya Y huwa ni nyepesi, husafiri kwa haraka katika via vya uzazi vya mwanamke na huishi kwa muda mfupi ukilinganisha na mbegu zenye vinasaba X.

Zenye vinasaba X huwa nzito zaidi, huenda polepole na huishi kwa muda mrefu zaidi.

Hivyo, kinadharia ili kupata mtoto wa kiume unaweza ukakutana na mwenza wako siku ambayo yai la uzazi linatoka (ovulation), kwani mbegu Y zitasafiri haraka na kukutana na yai ili kulirutubisha kuwa mtoto wa kiume.

Mtoto wa kike Mtoto wa kike, kutana na mwenzi wako (Siku za kupata mtoto wa kiume ) siku 2 au 3 kabla ya yai kutoka.

Kwa sababu mbegu Y huishi kwa muda mfupi, nyingi zitakufa wakati zinasubiri yai huku mbegu X zikiwa kwa wingi mpaka siku yai linatoka. Yai likitoka mbegu X zitakuwa kwa wingi kuungana na yai kutunga mtoto wa kike.   Kiuhalisia, sio rahisi kufanikisha hilo.  

Njia Nyingine Kuna njia mbalimbali zinazosemekana zinaongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume au wa kike.

Landrum Shettles, na iliyoainishwa katika kitabu nyuma katika miaka ya 1980. Njia hiyo inategemea nadharia ya kuishi kwa manii.

kupata mtoto wa kiume, dhana inasema, wanandoa wajitahidi kukutana kimwili siku nne mpaka sita kabla ya ovulation. Mbali na kuwa na rekodi za kuonyesha njia hii inafanya kazi, wakosoaji wanasema kufanya tendo la ndoa siku nne mpaka sita kabla ya yai kupevuka ni mbali sana na mara nyingi mbegu zilizobeba jinsia ya kiume haziishi mda mrefu.

Mikao wakati wa kujamiana

Zipo mbinu nyingi kuhusu aina fulani ya mikao itakusaidia kupata mtoto wa kike au kiume, lakini ijulikane kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha hivyo, lakini pia hakuna madhara ikiwa wewe na mwenza wako mkajaribu. 

Mikao inayoruhusu uume kupenya kwa kina ndani ya uke (deep penetration),itasaidia kupata mtoto wa kiume wakati mikao ile isiyoruhusu upenyo wa kina inasaidia kupata ujauzito wa mtoto wa kike (shallow penetration). 

Wataalamu wa mambo ya uchaguzi wa jinsia wanashauri ili kupata ujauzito wa mtoto wa kike mwanamke anatakiwa asifike kileleni. Mwanamke akifika kileleni anatoa alkali ambayo inasaidia mbegu zilizobeba jinsia ya kiume kuishi zaidi kwa kutengeneza mazingira yasiyohatarishi. Bila alkali hii inayotolewa pindi mwanamke amefika kileleni, mbegu zilizobeba jinsia ya kiume hushindwa kuishi na zina nafasi ndogo ya kufika kwenye yai lililotolewa na ovari tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke akifika kileleni inaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.

VIDOKEZO VINGINE IKIWA UNAJARIBU KUPATA MTOTO WA KIKE NI PAMOJA NA:

Kukutana na mwenza wako kimwili mara kwa mara. Punguza chumvi katika milo yako.  Kula vyakula vyenye asidi nyingi (machungwa, machenza,n.k) Nakuepuka vyakula vyenye alkali kama vile tango, tofaa, parachichi na almond. 

Mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume haziwezi kuishi katika mazingira yenye aside, hivyo kuongeza wingi wa aside mwili kupitia chakula kunasaidia kubadilisha kiwango cha Ph ya uke wako. Vilevile ikiwa mnatafuta mtoto wa kiume ulaji wa vyakula vyenye alkali ya kutosha utasaidia kuishi vizuri kwa mbegu zilizobeba jinsia ya kiiume.


JE, NIVYAKULA GANI VITAONGEZA NAFASI YA KUPATA MTOTO WA KIKE?

Vyakula vinavyofikiriwa kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kike ni pamoja na:

Maharagwe

Mboga za majani zenye kijani kilichokolea

Almond

Vyakula vya baharini hasa dagaa

Bidhaa za maziwa kama vile jibini, maziwa na mtindi

Bamia

Matunda jamii ya machungwa

Mayai

Karanga ya kusaga

Korosho

Mbegu kama mbegu za maboga na chia

Spinachi

Shayiri

Apple

Matunda kama strawberi,zabibu. 


JE, NIVYAKULA GANI VITAONGEZA NAFASI YA KUPATA MTOTO WA KIUME?

Vyakula vinavyofikiriwa kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume ni pamoja na:

Vyakula vyenye potasiamu ya kutosha kama vile ndizi, parachichi,uyoga,apple,almond, samaki aina ya salmon. 

Vyakula vyenye alkali ya kutosha kama vile machungwa, machenza,

Matunda freshi na mbogamboga

Nafaka nzima ambazo hazijakobolewa. Epuka bidhaa za maziwa.

KUMBUKA

Kwa kadri unavyotamani kupata mtoto wa kike au wa kiume, ukweli ni kwamba hakuna njia inayoweza kuahidi matokeo unayotaka. Na ukweli ni kwamba, hakuna madhara katika kujaribu njia hizi – lakini utafiti zaidi unahitajika ili kuthibitisha ufanisi wa mapendekezo haya. 

Bila kujali kama utapata mtoto wa kike au kiume, jambo muhimu ni kupata ujauzito salama na kujifungua mtoto mwenye afya.

kupata mtoto wa kiume, dhana inasema, wanandoa wajitahidi kukutana kimwili siku nne mpaka sita kabla ya ovulation. Mbali na kuwa na rekodi za kuonyesha njia hii inafanya kazi, wakosoaji wanasema kufanya tendo la ndoa siku nne mpaka sita kabla ya yai kupevuka ni mbali sana na mara nyingi mbegu zilizobeba jinsia ya kiume haziishi mda mlefu.

Chapisha Maoni

0 Maoni