Ticker

6/recent/ticker-posts

MAGONJWA 12 YANAYOTIBIKA KWA BINZARI MANJANO.


MAGONJWA 12 YANAYO TIBIWA KWA BINZARI MANJANO.

Binzari manjano asili yake ni Mashariki ya mbali, na  Tanzania hulimwa zaidi Mikoa yenye nyuzi joto 24-26`. Mikoa hiyo ni: Tanga, Kilimanjaro, Kagera, Morogoro, Kigoma na Zanzibar.

Kitaalamu hujulikana kwa jina la Curcuma_domestica na Kiingereza hujulikana kama Turmeric na Kiswahili huitwa  Binzari_Manjano , ambapo zao hili hustawi zaidi maeneo ya Mwambao na sehemu zenye umandeumande.

Kwenye Binzari manjano kuna Protini, Mafuta, Madini, Nyuzinyuzi, Kabohidreti, Calcium, Phosphorus, Carotine, Thiamine, Niacin na Madini ya Chuma.

Binzari_Manjano kitaalamu imethibitika kutibu magonjwa mbalimbali kama:- Minyoo, Surua , Upungufu wa damu (Anaemia) na kuondoa  Asidi tumboni kwa kuchanganya na chumvi kidogo na maji ya uvuguvugu.  Huweza pia kutibu Asuma ukichanganya na Maziwa Fresh.

Ukichanganya na Asali huweza kutibu Maumivu ya koo, Baridi yabisi (common cold), Kikohozi kikavu, Hysteria, Maumivu ya Viungo, Kisukari, Upungufu wa Nguvu za kiume, na Kupandisha kinga ya mwili.

Inauwezo pia wa kutibu  Macho (mtoto wa jicho) Majipu, Upele, Vidonda, Magonjwa ya Ngozi, Maumivu ya misuli,

Kuharisha damu, Lehemu, Kibofu na matatizo ya Kifua, Kushusha shinikizo la juu la damu (HBP), kusafisha Damu, Kuondoa matatizo ya nyongo na Magonjwa ya Ini.

Pia hufanya Ngozi ya mwili kuwa nyororo (hii ni kwa kuchanganya na sandalwood na kujipaka mwilini-wapo baadhi ya wadada hujipaka usoni kama scrub lakini hawajui uhalisia wake mwingine).

Ukiumia na damu inazidi kuvuja tia unga huu itakaka, Watoto wanaokua wapewe unga huu katika maziwa kila siku itasaidia ukuaji wao na kuimarisha mifupa, kusafisha damu na kusaidia mmeng'enyo wa chakula tumboni.  pia kuzibua pua zinazoziba mara kwa mara (blocked nose).

Binzari manjano, hutumika kwenye mishkaki, samaki, kuku, pamoja na mapishi mengine. watu wa pwani na tanga wanajua zaidi.

TAHADHARI:

Unaponunua binzari manjano uwe mwangalifu kwani binzari nyingi zilizo kwenye soko zimechanganywa na vitu vingine visivyofaa kwa afya ya Binadamu: Hivyo nzuri ni zile zinazovunwa moja kwa moja Mashambani. Iliyo halisi inakuwa imekoza rangi ya manjano sana na kuwa na harufu nzuri ya binzari manjano.

MATUMIZI YA MANJANO.


Wataalamu waliobobea kwenye fani ya tiba asilia wamethibitisha, ikiwa utaichemsha manjano kwa dakika 10 kwenye maziwa halisi ya ng'ombe, inakuwa sawa na antibiotics.

Mchanganyiko huo unaleta nguvu ya kutibu maradhi mbalimbali kama figo kushindwa kufanya kazi.

Figo ni tatizo linaloweza kutibika kwa kutumia maziwa na manjano. Kufeli kwa figo husababishwa na mambo mengi sana, baadhi yake ni kuubana mkojo kwa muda mrefu, kutokunywa maji ya kutosha na kutumia chumvi nyingi.

Baadhi ya visababishi vingine ambavyo vinaepukika ni kula nyama nyekundu mara kwa mara, kutokula chakula cha kutosha, kuchelewa kujitibu maambukizi madogo madogo na kutumia dawa za maumivu bila maelekezo.

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke ni tatizo linaloweza kutibika kwa kutumia maziwa na manjano.

Tatizo hili hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ya ndani ama nje ya mayai ya mwanamke.


Uvimbe huu unajulikana kwa jina la ‘Ovarian Cyst.’

Hutokea kwa wanawake wa umri wowote na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.

Tatizo hili linaweza kutibiwa kwa kunywa manjano yaliyochemshwa kwa kuchanganya na maziwa.

Kukosa choo

Mchemsho wa maziwa na manjano unatibu tatizo la kukosa choo. Kitaalamu kukosa choo kwa siku moja, siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kuwa na tatizo hilo iwapo atakosa choo zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.

Ni vizuri binadamu akipata choo mara tatu ndani ya saa 24.

Waswahili husema ‘raha ya nyumba ni choo’ hii ni kweli, hawajakosea kwa kuwa chakula chochote kinapoliwa lazima kitumike mwilini na mabaki yake yatolewe kupitia njia ya haja kubwa.

Ugumu wa kuitoa haja kubwa husababisha maumivu makali na pengine kuzalisha maradhi mengine kama bawasiri, kuumwa kichwa na homa.

Tatizo la kutopata choo linatokana na haja kubwa kwenda taratibu hivyo kuchelewa kutoka kwa wakati mwafaka. Dalili za kuwa na tatizo ni mgonjwa kupata maumivu ya tumbo ambayo hutokana na tumbo kujaa gesi.

Mtu mwenye tatizo la kukosa choo mara nyingi tumbo lake huvimba na kujaa gesi muda wote, hali hii inatokana na kuwa na uchafu tumboni.

Mwenye tatizo hili anywe manjano yaliyochemshwa kwa kuchanganya na maziwa.

Sanihealth ni chaguo lako sahihi katika kutatua changamoto mbalimbali za ki-afya. Mwananchi. Fikiri Tofauti.Tumekufikia. kwa lengo la kukusaidia pia tunaangalia namna ya kuboresha huduma zetu. Tafadhari tufahamishe nini ulichopendezewa nacho na nini tuboreshe zaidi.

Manjano mbichi ukichanganya na asali mbichi una kunywa dawa nzuri ya kusafisha mwili, 

Manjano mbichi na asali ukinywa ni dawa ya shinikizo la damu liwe la chini au la juu,

Manjano mbichi na asali ni dawa ya kuondoa mafuta (corestol) ndani ya mishipa ya damu


Manjano mbichi na asali, husaidia kuzuia ugonjwa, wa kupooza (kiharusi), 

Manjano mbichi, unga wa habbatt soda na asali ghafi ni mfumo wa dawa kwa wale ambao wana matatizo haya, 

Manjano mbichi na habbatt soda husaidia kuondoa Matatizo ya vidonda vya tumbo (Alsaas), 

Binzari manjano mbichi na yai la kuku, linalinda ngozi yako na kuiweka laini, pia kuilinda na kula Buddhist, ya jua kuchoma, 

Binzari manjano na yai la njano la kuku la ndani, husaidia kama unakabiliwa, na pentils, 

Watu wa vijijini mbali na hospitali, ikiwa umekatwa na kisu, upanga, spade, na poda ya njano, poda ya tumeric, juu ya majeraha husika kuzuia damu kutoka (clot) kama ya kwanza, 

Binzari manjano na habbatt soda kwa kutumia kikombe cha nusu cha kawaha, unawezesha mfumo wako wa fahamu kuwa bora na wenye afya,

Hizi ni baadhi ya faida za binzali manjano kwa maswali zaidi coment hapa chini kwa huduma nyingine bonyeza kitufe cha whatsApp hapo chini kulia kwako.

Chapisha Maoni

0 Maoni