NINI MADHARA YA UKAVU UKENI NA CHANZO CHAKE NI KIPI?Uke umeumbwa kwa mashavu yenye kuta zenye tishu laini sana. Na kufunikwa na majimaji yenye utelezi ili kusaidia mbegu za kiume kuogelea vizuri na kurutubisha yai wakati wa tendo la ndoa.
Uteute huu pia ni kilainishi cha uke kupunguza msuguano wakati wa tendo la ndoa.
Uzee Na Mashavu Ya Uke Kusinyaa
Kadiri mwanamke anavyozeeka mabadiliko ya uzalishaji wa vichocheo ama homoni hupungua na kupelekea kuta za uke kusinyaa na kuwa dhaifu. Kuta zikisinyaa maana yake seli zinazozalisha uteute zinapungua na hivyo kupelekea ukavu ukeni.
Mabadiliko ya homoni ndio sababu kubwa inayokufanya uwe na uke mkavu.
Nini Madhara ya Ukavu Ukeni?
Kukauka kwa uke wako kunaweza kusababisha madhara kama:-
kuhisi hali ya kuungua ndani ya uke kukosa hamu ya tendo la ndoa maumivu makali wakati wa tendo la ndoa kutokwa damu baada ya tendo kutokana na msuguano kuugua UTI kurahisi na kuwa sugu muwasho ukeni na
kuvimba kuta za uke.
Nini Kinapelekea Ukavu ukeni?
Kupungua kwa homoni ya estrogen ndicho chanzo kikubwa cha ukavu ukeni.
Wanawake wote hupungua uzalishaji wa estrogen kadiri wanavozeeka na kukaribia kukoma hedhi yaani menopause.
Menopause siyo chanzo pekee kwani kuna vitu vingine vinavyopelekea uwe na uke mkavu. Mambo mengine yanayopunguza uzalishaji wa estrogen ni pamoja na:-
kunyonyesha
kuvuta sigara
upasuaji kuondoa mifuko ya mayai(ovary)
stress kupita kiasi
mazoezi makali sana
sonona
magonjwa ya kinga na
baadhi ya tiba kama chemotherapy na radiotherapy.
Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?
Ni mara chache sana ukavu wa uke iwe ni kiashiria cha tatizo kubwa la ki-afya. Muhimu ni kutafuta ufumbuzi wa kidaktari endapo tatizo lako limechukua muda mrefu zaidi ya siku 30 .
Endapo usipotibiwa mapema ukavu wa uke unaweza kusababisha kumeguka kwa kuta za uke.
Matibabu ya Tatizo la Ukavu Ukeni. Kuna aina nyingi za tiba ambazo unaweza kuzipata famasi ya karibu yako ili kulainisha uke. Tiba hizi zinakuwa kwenye mfumo wa jelly mfano KY jelly ni maarufu sana.
USHAURI
Hakikisha unatumia vilainishi vya maji siyo vya mafuta. Vilainihsi hivi visiwe na manukato wala kemikali hatarishi.
Kamwe usitumie mate kama kilainishi wakati wa tendo la ndoa kwani unaweza kupata maambukizi ya bakteria. Usitumie mafuta ya kujipaka kama kilainishi kwani utaharibu kuta za uke.
Nawezaje kuzuia tatizo hili kujitokeza mara kwa mara?
Kunywa maji ya kutosha kila siku.
Usitumie sabuni wa marashi ukeni.
Ongea na mwenzi wako kuhusu tatizo hili akuvumilie wakati unatafuta tiba.
Je kuna madhara yoyote kutumia jelly na vilainishi vya pharmacy?
Ndio, vilainishi hivi vya kununua pharmacy siyo vya kuvizoea kama tiba ya tatizo. Vitumike mara moja moja sana ama kuacha kabisa kuvitumia.
Madhara yake ni makubwa endapo zinatumika kwa mda mrefu. Athari hiyo ni kuvurugika kwa mazingira ya uke na kuugua fungus na kutoa harufu mbaya ya uke pia huwauwa bakteria wazuri walinzi wa uke na kutokwa na uchafu usio wa kawaida.
Ndiomana tunashauri kulenga kutibu chanzo cha tatizo ambalo ni kurekebisha homoni.
Tumia Vidonge Asili vya Yunzh feminine kurejesha uteute mzuri.
Yunzh feminine crence ni tiba asili iliyo kwenye mfumo wa vidonge. Na maji Ni dawa zinazozalishwa nchini malekani kutibu changamoto za wanawake kama ukevu ukeni, upungufu wa ute, hedhi kuvurugika na maumivu makali kwenye hedhi.
Dozi moja ina vidonge 30, unatumua kwa week mbili. Kulingana na ukubwa wa tatizo lako tunaweza kushauri utumie zaidi ya dozi moja.
Gharama ni Tsh 150,000/= Tuma ujumbe whatsapp no: 0658091941 kuanza Tiba.
Sani afya ni darasa la elimu ya afya ya magonjwa kupitia mtandao.
Lengo ni kuwafikia watu wengi zaidi afrika mashariki kupitia elimu ya magonjwa na kuwakutanisha na wataalamu wa afya katika kipindi kigumu cha maambukizi ya bakteria wa magonjwa aina mbalimbali.
0 Maoni