Ticker

6/recent/ticker-posts

HATUA ZA UKUAJI WA UJAUZITO NA MTOTO


HATUA MUHIMU ZA UKUAJI WA UJAUZITO NA MTOTO

Ujauzito umegawanyika katika hatua kuu tatu, au vipindi vikuu vitatu ambavyoni:-

1.TRIMESTER YA KWANZA (FIRST TRIMESTER). 


Hiki ni kipindi katia ya wiki 1 mpaka 12 yaani ndani ya miezi mitatu ya kwanza. 

Kipindi hiki mjamzito awe makini sana kwani ni kipindi ambacho kutoka kwa ujauzito ni rahisi sana. Kipindi hiki ndicho ambacho mtoto anaanza kukuwa ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine kama moyo na masikio. 

Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 75 ya mimba zinazotoka huwa zinatoka katika kipindi hiki. Hata kwa wanaotowa mimba pia hutoa katika kipindi hiki.

Mabadiliko ya mwili katika kipindi hiki.

A.Uchovu

B.Kukosa haja kubwa

C.Kichefuchefu

D.Maumivu ya kichwa

MAMBO HATARI KATIKA KIPINDI HIKI.


A.Wacha kuvuta sigara

B.Wacha kunywa pombe

C.Wacha kutumia dawa kiholela bila ya ushauri wa daktari.     D.Kuwa makini sana kwani kosaadogo ujauzito upo hatarini.    E.Punguza kuchwa chai kupitiliza.   F.Punguza kula samaki kwenye magobeta jaamii ya tondo.



2.TRIMESTER YA PILI (SECOND TRIMESTER)

Kipindi hiki ni kati ya wiki 13 mpaka 27 yaani kuanzia mwezi wa 3 mpaka wa 6 kwenda wa saba. Katika kipindi hiki mwanamke atafanyiwa vipimo vya utrasound kuangalia mkao wa mtoto na kama yupo katika afya njema. Katika kipindi hiki hata jinsia ya mtoto itaweza kuonekana kwa ambaye anataka kufahamu kupitia  kipimo cha utrasound. Hapa mtoto anaweza kuishi nje ya mwili wa mama yake kuanzia wiki ya 23. na endapo mtoto atazaliwa hapa atakuwa njiti hivyo vifaa maalumu vitahitajika kumlea kabla ya kuanza kuishi huru. Katika kipindi hiki mama mjamzito atasikia vurugu za mtoto tumboni, kupiga mateke, kugeuka na kuhama katika sehemu moja na kwenda nyingine.

Katika kipindi hiki karibia dalili zote za ujauzito za mwanzo hupotea. Nguvu inarudi vyema na utaweza kulala usingizi mnono usiku. Katika kipindi hiki tumbo litaanza kuonekana kukuwa zaidi. Katika kipindi hiki jiepushe sana na yafuatayo:-

A.Kuvaa nguo za kubana

B.Kuwa na hasira mara kwa mara. Yaani jitahidi kutafuta furaha, kaa na marafiki cheka na ufurahie.

C.Usijibane tumbo hata kama litakuwa kubwa zaidi.

Katika kipindi hiki unaweza kuhisi kiungulia mara kwa mara, na maumivu ya miguu. Hamu ya kula inawea kuongezeka zaidi, na uzito pia kuongezeka katika kipindi hiki. 

Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya mgongo. Hata hivyo anaweza kujihisi kama una mafua ama pua zimeziba ila ukifina hakuna kitu. Pia unaweza kuiona mishipa inatokeza kwa nje hasa kwenye miguu.

Katika kipindi hiki mama mjamzito ataanza kusikia mijongeo ya mtoto. Hata hivyo mtoto ataweza kuitambua sauti ya mama yake na watu wa karibu sana na mama yake. 

Baadhi ya viungo vinavyoweza kuonekana kwenye utrasound katika kipindi hiki ni kama figo, mapafu, moyo na ubongo na jinsia. Katika kipindi hiki mama mjamzito anaweza kupimwa kisukari cha mimba kuanzia wiki ya 26 mpaka 28.


3.TRIMESTER YA TATU (THIRD TRIMESTER).

Kipindi hiki huanzia wiki ya 28 mpaka 40, yaani kuanzia miezi 7 kwa makadirio. Katika kipindi hiki mara kwa mara utahitajika kumuona daktari kwa vipimo zaidi. Daktari atakuwa anakuangalia maendeleo yako kwa jumla na afya ya ujauzito wako. Atakuwa anakucheki:-

A.Anapima mkojo kuangalia protini. 


B.Atakuwa anakuangalia shinikizo la damu (presha)

C.Atasikiliza mapigo ya moyo wa mtoto.

D.Atakuwa akipima njia ya uzazi atakuwa anacheki miguu na mikono kama itakuwa inavimba.

Pia daktari anaweza kukupima uwepo wa bakteria wanaoitwa Group B streptococcus (GBS) kwenye uke. Uwepo wa bakteria hawa unaweza kuhatarisha afya ya mtoto anayezaliwa. Katika kipindi hiki ni vyema kuanza kufuatilia habari za kujifungua, mazoezi ya kujifungua na namna ya kujiandaa.


BAADA YA KUJIFUNGUA.

Watoto wachanga wana uzito wa kilo 7.5. Madaktari hutathmini hisia za mtoto mchanga, kama vile kunyonya, mizizi, na reflexes ya Moro. Ujuzi wetu wa kimwili, kiakili na kisaikolojia hukua na kubadilika kadiri tunavyosonga mbele katika hatua za ukuaji kutoka utoto hadi utu uzima. 


Kushikamana katika utoto ni sehemu muhimu ya ukuaji wa afya. Mitindo ya uzazi imeonekana kuwa na athari juu ya matokeo ya utoto ya ustawi. Mpito kutoka ujana hadi utu uzima unaweza kuwa na changamoto kutokana na muda wa kubalehe, na kutokana na muda ulioongezwa unaotumiwa katika utu uzima unaojitokeza. Ingawa kushuka kimwili huanza katikati ya utu uzima, kupungua kwa utambuzi huanza baadaye. 

Shughuli zinazoweka mwili na akili hai zinaweza kusaidia kudumisha afya nzuri ya mwili na utambuzi kadri tunavyozeeka.   Usaidizi wa kijamii kupitia familia na marafiki hubaki kuwa muhimu kadri tunavyozeeka.

Chapisha Maoni

0 Maoni