Ticker

6/recent/ticker-posts

AINA ZA VYAKULA VINAVYO SAIDIA KUSHIKA UJAUZITO HARAKA.

 


AINA ZA VYAKULA VINAVYO SAIDIA  KUSHIKA UJAUZITO HARAKA.

Unajumuisha vyakula vitakavyosaidia mfumo wako wa uzazi kwa kuimarisha na kusimamia upevushwaji wa mayai na kuboresha nafasi ya kushika mimba pi katika kujifungua salama.

Mlo huu unampatia mtoto mwanzo mzuri wa maisha yake na ubongo wenye afya. virutubisho muhimu ambavyo ni muhimu katika kuimarisha mfumo  wa uzazi kwa mwanamke na mwanaume :

Beta-carotene, phytonutrient, inaimarisha homoni na kuboresha uwezo wa mwanaume kumpa mwanamke ujauzito. Vitamin B zinazosaidia mfuko wa mayai wakati wa kupevushwa yai na pia kusaidia kuepuka mimba kuharibika. 

Foliki asidi inasaidia kuepuka matatizo ya neva za fahamu kwa mtoto atakayezaliwa.

Vitamin C inasidia kufyonza homoni ya pogesteroni na kumsaidia mwanamke na kasoro za lutea (luteal phase defects).

Vitamin D inasaidia kuboresha uwezo wa kuzaa kwa wanandoa wote.  Inachukua jukumu kuu la kutibu matatizo ya uzazi kama uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, uvimbe kwenye mfuko wa mayai, na kuboresha mbegu za kiume kwa mwanaume.

Vitamin E inakuza afya ya yai na mbegu za kiume.Madini ya chuma yanapunguza nafasi za ugumba unao sababishwa na yai kushindwa kupevushwa.

Omega 3 na asidi za fati zina saidia kuboresha idadi ya mbegu za kiume na uwezo wake wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine vilevile na kuongeza kasi ya damu kwenye mfuko wa uzazi. Antioxidants zina kinga na kutibu ugumba.

Zinki na selenium zinaimarisha ubora wa mbegu za kiume. Vyakula vyenye fati nyingi vinaweza punguza hatari za ugumba unao sababishwa na yai kushindwa kupevushwa. Vifuatavyo ni vyakula unavyoweza kuongeza kwenye mlo wako:

1. Mbogamboga za majani. Mbogamboga za majani kama spinachi zina utajiri wa vitamini C na foliki asidi. Pia zinasaidia kuboresha upevushwaji wa yai, utengenezaji wa mbegu za kiume nzuri na kupunguza nafasi ya mimba kuharibika au magonjwa ya kurithi.

Broccoli: zina wingi wa vitamin C ambayo ni muhimu kwenye upevushwaji wa yai Kabichi: ni chakula kizuri kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi. Pia ni chanzo kizuri cha Di-indole methane, ambayo inasaidia kumkinga mama na uvimbe wa mfumo wa uzazi na endometriosis. Viazi:  wingi wa vitamin C na kutibu kasoro za lutea kwa mwanamke.

Nyanya:  Zina wingi wa lycopene, inayosaidia kuboresha idadi ya mbegu za kiume na kuongeza kasi ya mbegu kuogelea.Karoti: chanzo kizuri cha beta-carotene Viazi vikuu:  Vina phytoestrogens, ambazo zinahamasisha utoaji wa yai kutoka kwenye mfuko wa mayai na kusaidia kutibu kasoro za lutea kwa wanawake.

2. Matunda Matunda ni chanzo kizuri cha antioxidants, ambazo ni muhimu katika kuzaa. Mfano wa matunda hayo ni: Komamanga:  chanzo kizuri cha vitamini C, na inasaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.

Parachichi:  Iina wingi wa vitamin B ambayo ni muhimu katika ukuaji wa seli na mfumo wa uzazi, vitamin E,nyuzinyuzi, madini na mafuta muhimu. Vitamin E inasaidia kutunza ukuta wa mfuko wa uzazi.

Banana: ina wingi wa vitamin B6 na potasiamu. Inasaidia kuboresha uwezo wa kupata ujauzito kwa kusimamia homoni na kuimarisha ubora wa yai na mbegu za kiume. Zabibu na machungwa yanasaidia kuboresha afya ya yai kwasababu ya wingi wa “polyamine putrescine” ndani yake.

Nanasi:  kuna imani inayofuatwa inayoaminika kwamba ukila mzizi wa katikati ya nanasi unamsaidia mwanamke kushika mimba kwa siku tano za yai kupevushwa au wakati mbegu imepandikwa ndani ya mwili wa mwanamke kwa njia ya IVF. 

Nanasi pia lina wingi wa vitamin C inayosaidia kukuza nafasi ya kupata ujauzito kwa mwanamke na kupunguza hatari ya uvimbe kwenye ovari. 

Nanasi linakuza ubora wa mbegu za kiume kwa wavutaji sigara.

3. Vyakula visivyo mbogamboga

Vyakula hivi ni kama nyama, samaki, na mayai ambavyo vina wingi wa omega3-fati asidi. Mayai:  yana wingi wa omega-3, foliki aside na vitamin D.Salmon:  ana wingi wa omega 3 fati asidi.Nyama( kuku/nyama): ni chanzo kizuri cha chuma,na fati muhimu.

4. Bidhaa za maziwa

Zina wingi wa kalsiamu, fati nzuri,na vitamin D, bidhaa zitokanazo na maziwa ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa kupata ujauzito kwa wanandoa ambao wanataka kuwa na watoto haraka. 

Zifuatazo ni baadhi ya bidhaa muhimu za maziwa:  Maziwa yana wingi wa kalsiamu na fati nzuri. Yogurt:  chanzo kizuri cha kalsiamu,probiotics, na vitamin D.

5. Miti shamba na viungo

Hii inasaidia kuendeleza usawa wa homoni ya estrojeni kwa mwanake na kusaidia uwezo wa kupata ujauzito.

Binzari: Ina wingi wa antioxidants na inasaidia kutibu matatizo yote yanayohusiana na hedhi.

Kitunguu swaumu:  ni kiungo kinachokuza uwezo wa kushika mimba na kina antioxidant inayosaidia mbegu za kiume kusafiri kwa haraka na kuongeza nafasi ya kupata ujauzito ikiwa utatumia siku tano zote za kupevushwa yai. 

6. Mafuta na mafuta ya mbegu.Mbali na mbogamboga, matunda, na nyama mbegu na mafuta yake yanachukua jukumu kubwa katika kuboresha nafasi ya kushika mimba.  Baadhi ya mafuta hayo ni kama:

Mafuta ya Olive: Yanatoa fati zilizo muhimu katika mwili zinazosaidia kupunguza kuvimba mwili kwa ndani na kuongeza umakini wa insulini ndani ya mwili wa mwanamke. Inaboresha nafasi ya kupata ujauzito kwa wanawake waliopandikiza mtoto(IVF)

Mbegu za maboga: 

Zina wingi wa zinki ambayo inasaidia kusimamia afya ya mfumo wa uzazi.  Pia zinki inasaidia kuongeza viwango vya homoni ya testosteroni na mbegu za kiume na kuimarisha mtiririko wa damu kwenye ogani za mfumo wa uzazi. 

Zinki inasaidia kuzalisha mayai yaliyokomaa. Mbegu za alizeti, zina wingi wa zinki.

7. Matunda makavu

Almond: wingi wa vitamin E na omega-3 fati asidi. Njugu: zina wingi wa omega-3 fati, magnesiamu na nyuzinyuzi zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula.  Zinaboresha nguvu za manii na spidi yake pia. 

8. Vyakula vingineKunde na maharagwe: Yana utajiri wa protini, nyuzinyuzi na vitamin B.

Nafaka: kama mchele wa kahawia,mtama, ngano nk.  Hizi zina wingi wa nyuzinyuzi na husimamia kiwango cha sukari, hivyo kuendeleza kiwango cha foliki aside ili kukuza nafasi ya kupata ujauzito.

VYAKULA VYA KUVIEPUKA WAKATI WA KUTAFTA UJAUZITO.



Vyakula vyenye mabaki ya dawa za viwandani za kukuza mazao, kama strawberi, sukumawiki, pilipili, au zabibu, vinapunguza nafasi ya kupata ujauzito.  Vyakula vya baharini kama samaki wa maji chumvi, walio na mekyuri nyingi. 

Mekyuri nyingi inapelekea ugumba na kuharibika mimba. Vyakula vinavyopitishwa kwenye mafuta kama vyakula vya kuoka,vya kukaanga na viwandani. Vyakula vyenye kabohaidreti ulaji wa kabohaidreti ndogo unaweza kuongeza ugumba kwa kuhatarisha viwango vya insulini na “testosterone”. 

Lakini pia vyakula vyenye sukari na nafaka zilizokobolewa zinaweza kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu na kusababisha ugumba unaosababishwa na yai kushindwa kupevushwa.Kwa wale mliopata tiba tayari hapa kama mnanawatu kwa majibu yenu baada ya siku 60 baada ya matumizi ya dawa zenye kilakitu nilicho kitaja hapo juu.Kwa wale ambao bado hujatumia tiba endelea kutumia vyakula ainahizi mfululizo ndani ya siku 90 mungu ataleta wepesi utafanikiwa kupata ujauzito.


USHAURI KWA WANA NDOA WANAOTAFTA UZAZI.


Hkikisha unazingatia aina za lishe zinazo hitajika wakati wa kutafta ujauzito pamoja na kuepuka aina zote za vyakula na vinywaji hatari kwa utungishaji wa mimba.  Kama utatumia njia hii zaidi ya siku 90 bila ya mafanikio hakikisha unawakilisha hisia zako kwa mshauri wa afya kupata ushauri zaidi.

Kama utahitaji matibabu ya ziada kwaajili ya kusaidia mwili wako kupata muitikio wa kunasa ujauzito ipo dawa kwaajili ya wana ndoa wenye uhitaji wa kufanikiwa kwa haraka. Kumbuka ujauzito hutungwa kwa muunganiko wa jinsia mbili tofauti pia kutegemeana na uimara wa jinsia zote mbili hivyo unapaswa kuandaa lishe nzuri kwaajili ya mume  lishe nzuri ambayo ni rafiki kwa kuongeza mbegu za kiume.


HITIMISHO LA TIBA KWA WANANDOA MKE NA MUME.



Jambo la kushukuru ni kwamba  pamoja na wanandoa wengi kukabiliwa na tatizo la uzazi lakini ukweli ni kwamba tiba ipo kutegemeana na chanzo cha tatizo mara nyingi wanandoa wengi wamekuwa wakikosa ushilikiano na kusababisha wimbi kubwa la ugumba kwa wanandoa wengi baadhi yao hufikia hata kutarakiana kwasababu ya kukosa kubeba ujauzito.

Hata hivyo watafiti mbalimbali wamegundua baadhi ya vyakula hivi vya nyumbani ambavyo husaidia kuimarisha afya ya uzazi kwa pande zote mbili na kuamua kuunda mkusanyiko huo wa lishe kwa kufanya mchujo wa virutubishi muhimu na kuhifadhi kama tiba.

Kama wanandoa wataafiki na kukubaliana kupata matibabu haya ni vema wakachukua hatua mapema na kuanza tiba mapema namna ya kuipata tiba hii wasliana na mtalamu wa afya kuitia namba 0658091941

Napatikana Tunduma mpakani mkoa wa songwe kwa wale mliopo mikoa ya mbali natuma  kupitia mabasi ya mkoa na inakufikia mpaka ulipo kwa uaminifu mkubwa wa afya bora tanzania DR.SANI MLAWIZI.

Chapisha Maoni

0 Maoni