Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU CHANZO CHA KUVIMBA KWA MLANGO WA SHINGO YA UZAZI


KUVIMBA KWA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI. 


Shingo ya mlango wa kizazi ni nini?

Shingo ya kizazi au mlango wa kizazi ni eneo la chini kabisa kwenye kizazi chako. 

Hapa ndipo damu ya hedhi hutokea baada ya ukuta wa kizazi kubomoka. 

Wakati wa kujifungua leba shingo ya kizazi hufunguka ili kupisha mtoto azaliwe kwa njia ya uke. 

Shida ya kuvimba mlango wa kizazi inawatokea wanawake wengi sanaa.

Kama ilivyo kwa tishu zingine za mwili, tishu za shingo ya kizazi zinaweza kututumka na kuvimba pia kutokana na sababu mbalimbali. 

Kitaalamu kuvimba kwa shingo ya kizazi huitwa cervicitis.


DALILI ZA KUVIMBA MLANGO WA KIZAZI


1. Kuvuja damu kusiko baada ya tendo au wakati mwingine

2. Maumivu ukeni.

3. Kutokwa a uchafu wa kijivu na mweupe wenye harufu mbaya kwa muda mrefu.

4. Maumivu ya mgongo

kuhisi kama mgandamizo kwenye nyonga na kiuno kuwa kizito.

5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.


CHANZO CHA KUVIMBA KWA SHINGO YA KIZAZI.


Sababu kubwa inayopelekea kizazi chako kuvimba ni maambukizi. 

Maambukizi haya yanaweza kupatikana hasa kutokana na tendo la ndoa.

Kuvimba huku kwa kizazi tunaweza kuweka katika makundi mawili,

Acute cervicitis– ambapo dalili hujionesha haraka na kupotea na:-

Chronic cervicitis– ambapo dalili huchukua miezi mingi bila kupotea.

Kuvimba shingo ya kizazi husababishwa hasa na magonjwa ya zinaa kama:-

gonorrihea

chlamydia

trichmoniasis na

genital herpes.


Kuvimba kwa shingo ya kizazi pia kunaweza kusababishwa na maambukizi kutokana na sababu mbalimbali kama:-

Aleji ya kondomu

kitanzi.

Matumizi ya pedi ambazo siyo salaama ama tampon.

Maambukizi ya mara kwa mara ya bakteria ukeni.


VIPIMO VYA UVIMBE KWENYE SHINGO YA KIZAZI.


Kama una dalili za kuvimba kwa shingo ya kizazi, muhimu umuone daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

Kumbuka dalili hizi za kizazi kuvimba zinaweza kuashiria matatizo mengine makubwa zaidi ya ki-Afya.

Daktari pia anaweza kugundua kuvimba kwa shingo ya kizazi chako kama huwa unafanya vipimo hospitali mara kwa mara. 

Zifuatazo ni njia anazotumia daktari kufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi kuvimba.


BIMANNUAL PELVIC EXAM.


Kwenye kipimo hiki, daktari ataingiza kidole chake ukeni chenye glove, kisha mkono mwingine atabinya tumbo kwa nguvu. 

Hii itamsaidia daktari kugundua uvimbe wowote usio wa kawaida kwenye shingo ya kizazi.

PAP TEST

DR.ELYASI  0658091941 & 0782812300.


Kwenye kipimo hiki, daktari atachukua sampuli ya ute ute au uchafu wa ukeni, kisha atapeleka maabara kuufanyia vipimo kuona kama kuna shida.

CERVICAL BIOPSY.


Daktari anaweza kupendekeza kipimo hiki endapo kipimo cha pap test kimeonesha kuwepo kwa seli zenye tatizo. 

Wakati wa kipimo hiki daktari huingiza kifaa kinachoitwa speculum kwenye njia ya uke.

Kwa kutumia kifaa kingine kinachoitwa colposcope daktari atachunguza eneo la shingo ya kizazi, kisha atakata sampuli ndogo ya nyama kwenye eneo lililovimba na kupeleka maabara kwa vipimo.


CERVICAL DISCHARGE CALTURE.


Kipimo hichi ni cha kuotesha kuona kama una maambukizi ya fangasi aina ya candida. 

Daktari atachukua sampuli ya uteute wa ukeni kisha ataotesha kwa siku kadhaa na kuupima.

Tiba kwa tatizo la kuvimba mlango wa kizazi.

Hakuna tiba ya moja kwa moja ya kuvimba shingo ya kizazi kwa hospital. 

Daktari wako atakushauri tiba sahihi kulingana na chanzo cha tatizo lako, hali ya afya yako, historia ya tatizo, ukubwa wa tatizo na dalili zote unazopata.

Tiba kuu ni kupitia antibiotics kwa ajili ya kutibu maambukizi. 

Kama shingo ya kizazi imevimba kutokana na kutumia pedi, tampon au kitu chochote cha kuingiza ukeni basi suluhisho itakuwa ni kuacha kutumia kitu hicho.

Kama shingo ya kizazi imevimba kutokana na saratani, daktari anaweza kupendekeza uanzishiwe tiba ya mionzi ili kuua seli za saratani.

Bila kupata matibabu ya uhakika tatizo lako la kuvimba kwa shingo ya kizazi linaweza kuwa kubwa zaidi na kuleta maumivu makali zaidi wakati wa tendo.


MADHARA YA TATIZO LA  KUVIMBA KWA SHINGO YA KIZAZI.


Kuvimba kwa shingo ya kizazi kutokana na magonjwa ya zinaa hupelekea kusogea kwa ukuta wa kizazi na mirija ya uzazi na kusababisha maambukizi kwenye kizazi-P.I.D. 

P.I.D huongeza zaidi maumivu ya nyonga, kutoka uchafu mwingi na homa. 

P.I.D isipotibiwa mapema husababisha ugumba

.

JINSI YA KUJIZUIA KUPATA CHANGAMOTO YA KUVIMBA KWA KIZAZI?.


Kuna njia kadhaa zitakazo kusaidia kupunguza hatari ya kuvimba kwa shingo ya kizazi. 

Tumia kondomu kila mara unapofanya tendo na mtu usiyemwamini kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Usitumie bidhaa zenye kemikali, kama tampons za kunukia ili kupunguza aleji. 

Kama unatumia kitu chochote cha kuingiza ukeni mfano tampon, hakikisha unafuata maelekezo sahihi muda gani wa kukitoa na kujisafisha.


USHAURI.


tunazo tiba za kumaliza kabisa chanzo cha maambukizi katika mfumo wa uzazi pamoja na vimbe aina zote.

Ni tiba ASILI  ambazo ni aina ya mimea ya lishe mchanganyiko.

Huboresha kinga ya mwili na kutibu kabisa magonjwa sugu ya mfumo wa uzazi.

Kama unaona dalili yoyote kati ya hizo nilizozitaja hapo juu tuwasliane ili kupata tiba sahihi na yenye uhakika wa kumaliza tatizo bila kufanyiwa upasuaji..

Chapisha Maoni

0 Maoni