FAHAMU CHANZO CHA UGONJWA WA U.T.I DALILI NA TIBA YAKE
FAHAMU CHANZO CHA UGONJWA WA U.T.I DALILI NA TIBA YAKE.
U.T.I ni kifupisho cha Urinary Track Infection. Ni ugonjwa unaoshambulia katika mfumo wa mkojo, hususan kibofu, figo na mirija ya urethra. Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata zaidi wanawake kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 10 mmoja ana UTI.
Maambukizi ya ugonjwa huu yanapatikana hasa chooni. Pia maambukizi ya u.t.i huenezwa kupitia ngono kuingiliana kimwili na utaratibu mbovu wa kujisafisha baada ya kukidhi haya.
Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata zaidi watu ambao wanatumia vyoo vya shirika yaani vyoo vinavyotumiwa na watu wengi.
Ugonjwa wa u.t.i umekuwa ukisababishwa na bakteria kwa kiasi kikubwa. Bakteria aina ya E.coil ambao wanapatikana kwenye utumbo mkubwa bakteria hawa wamekuwa wakisababisha u.t.i kwa kiasi kikubwa kuliko bakteria wengine.
Pia fangasi (fungi) na virusi huweza kusababisha u.t.i japo kwa kiwango kidogo mtu anaweza kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa huu kwa,;-
1.Jisafishe kutokea mbele kuelekea nyuma baada ya kukidhi haja kubwa (kwa wanawake). Hii husaidia kuzuia bakteria wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wasipate nafasi ya kuingia kwenye njia ya haja ndogo.
2.mwaga maji kila uingiapo chooni kwaajili ya kujisaidia. Kitendo hiki kitasaidia kuondoa vijidudu vilivyopo pale chini.
3.Jisafishe sehemu za siri kabla ya kuingiliana na baada.
4.Hakikisha unakwenda kutoa haja ndogo (kukojoa) baada ya tendo la ndoa. Kitendo hiki kitasaidia kuondoa vijidudu vilivyoingia wakati wa tendo.
5.Nenda katoe haja ndogo haraka sana baada ya kuhisi mkojo.
6.Kunywa maji mengi zaidi. Husaidia kuondowa vijidudu kwa njia ya mkojo.
7.Vaa nguo za ndani za pamba, kavu na zisizobana.nguo za mpira na zinazobana husababisha jasho (majimaji) sehemu za siri. Majimaji haya husaidia bakteria kukuwa na kuishi hivyo wanaweza kuathiri njia ya mkojo.
Ugonjwa wa u.t.i una dalili nyingi na huenda nyingine zikafanana na dalili za malaria. Miongoni mwa dalili hizi ni;-
1.Maumivu wakati wa haja ndogo
2.Kutowa mkojo mchafu. Mkojo unaweza kuwa na rangi sana, ama kama wa mawingu.
3.Harufu kali sana ya mkojo.
4.Mkojo kuwa na damu
5.Kukojoa marakwa mara hata kama mkojo utakuwa ni mchache sana.
6.Maumivu ya mgongo na tumbo kwa chini.(lower abdomen)
7.Maumivu ya kichwa.
8.Kuhisi uchovu sana
9.Miwasho sehemu za siri.
Itambulike kuwa ugonjwa wa u.t.i unatibika bila ya matatizo. Jambo la msingi ni kuwa wagonjwa wengi wamekuwa hawatumii dozi zao kikamilifu.
Kwakuwa ugonjwa huu umeenea sana na ni rahisi kuupata imetokea hali za kujirudia rudia kwa baadhi ya wagonjwa.
Hivyo mgonjwa ni muhimu kuchukuwa tahadhari nilizo zitaja hapo juu wakati akiwa anatumia dozi. Pia watu wawe makini na tiba za kiasili ambazo husemekana zinatibu u.t.i.
DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU U.T.I
1. BAKING SODA
U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari.
U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi.
Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I.
Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka.
Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya hewa safii mwilini.
- ZABIBU NYEUSI (BLUEBERRIES) NA ZABIBU NYEKUNDU (CRANBERRIES):
Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria.
Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I.
Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. 3. NANASI
Nanasi Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo.
Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’.
Utafiti umeonyesha, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kumaliza kabisa maambukizi ya U.T.I.
Kula vipande 4 mpaka 6 vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu. 4. MAJI
Maji Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji.
Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano.
Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa. 5. VITAMINI C
Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini
Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo.
Vitamini C hufanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo.
Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye mlonge.
Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na kujitibu U.T.I. 6. KITUNGUU SWAUMU:
Kitunguu swaumu Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo.
Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo.
Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I. Namna ya kukitumia;
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2, menya nusu yake (punje 10 au 15), menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na mapema uamkapo asubuhi kwa siku 7. 7. LIMAO/NDIMU:
Limau/Ndimu Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limau au ndimu na uongeze maji ili kupata robo lita (ml 250) na unywe kutwa mara tatu.
Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake.
Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.8. UNGA WA MELONGE
Mlonge Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji, au ndani ya juisi ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali.
Tumia kwa mwezi mmoja mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa. 9. SHUBIRI (ALOE-VERA):
Mshubiri/Aloe Vera Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa vinne, changanya na maji ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 2 au hadi utakapopona. Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.
Katika dawa hizi zote zilizojadiliwa hapa, napendekeza utumie dawa hizi kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na kwa haraka, nazo ni; maji ya kunywa, kitunguu swaumu, limau, unga wa majani ya mlonge na mshubiri.
USHAURI.
Umejaribu kutumia tiba hizi lakini dalili bado zinaonyesha kuendelea unashauriwa umuone daktari ama kwenda kufanya vipimo ili kuthibitisha ukubwa wa tatizo.
Kwa maswalina ushauri zaidi coment hapa chini ama kutuma ujumbe mfupi whatsApp kwaajili ya kukata kiu yako na kujiridhisha zaidi. Dr.SANI MLAWIZI.
0 Maoni